{"id":7589,"date":"2025-03-17T18:09:48","date_gmt":"2025-03-17T18:09:48","guid":{"rendered":"https:\/\/website.zanrevenue.org\/?p=7589"},"modified":"2025-03-18T15:30:06","modified_gmt":"2025-03-18T15:30:06","slug":"wataalamu-wa-kodi-afrika-mashariki-wakutana-zanzibar","status":"publish","type":"post","link":"https:\/\/website.zanrevenue.org\/sw\/wataalamu-wa-kodi-afrika-mashariki-wakutana-zanzibar\/","title":{"rendered":"Wataalamu wa Kodi Afrika Mashariki Wakutana Zanzibar"},"content":{"rendered":"<ul class=\"wp-block-list\"><li><strong>Zaahidi kushirikiana, kutatua changamoto kwa pamoja<\/strong><\/li><\/ul><p><strong>Na Muandishi Wetu.<\/strong><\/p><p>MAMLAKA za Kodi za nchi za Afrika Mashariki, zimesema zitaendelea kushirikiana pamoja katika kutatua changamoto za kodi zinazofanana na kubadilishana uzoefu ambao utasaidia kuimarisha mapato ya nchi zao.<\/p><p>Kaimu Kamishna Mkuu wa Mamlaka ya Mapato Zanzibar (ZRA) Ndg. Saidi Ali Mohamed, alieleza hayo leo wakati akifungua mkutano wa 98 wa Kamati ya Wataalamu wa Mamlaka za Mapato za Afrika Mashariki ulioanza leo katika Ukumbi wa Hoteli ya Madinat Al Bahr iliyopo Mbweni nje kidogo ya mji wa Zanzibar.<\/p><p>Kamishna Said alisema watahakikisha wanajadiliana na kushirikiana katika kutafuta mbinu ambazo zitawezesha kutumiwa na nchi hizo na kuondosha tatizo hasa la kutokudai na kutokutolewa Risiti za kielektoriniki kwa wananchi ambao bado hawana muamko wa kuchukua risiti kila wanapofanya manunuzi.<\/p><p>Aidha alisema mkutano huo utajadili njia mbadala za kuondosha biashara za magendo kwa Nchi wanachama wa Afrika Mashariki kwani kuendelea kwa biashara hizo kunaathiri vibaya makusanyo ya Mapato.<\/p><p>Mbali na hayo Kamishna Said alisema ni matumaini yake kuwa mkutano huo utakuwa fursa ya kuimarisha lugha ya Kishwahili na wageni kujifunza lugha hiyo kwa sababu ni lugha adhimu ambayo inatambulika kimataifa sambamba na kuwaomba kutembelea vivutio vya kitalii vilivyopo Zanzibar.<\/p><p>Naye, Mwenyekiti wa Kamati ya Wataalamu wa Mamlaka za Kodi za Afrika Mashariki Ndg. Beatus Nchota, alisema Mamlaka za Kodi za Afrika Mashariki zinakabiliwa na ukwepaji wa kodi hususan katika bidhaa za Forodha hivyo mkutano huo utabainisha bidhaa ambazo zinakwepa kodi zaidi kwa kuelezea sababu zao na hatimaye kuzipatia ufumbuzi.<\/p><p>Kwa upande wake, Mkurugenzi kutoka Idara ya Utafiti na Mipango ZRA Ndg. Ahmed Haji Saadat, alisema kupitia mkutano huo Wawakilishi kutoka ZRA watajifunza uzoefu kutoka kwa Mamlaka nyengine za Kodi za Afrika Mashariki na kupata majibu ya changamoto zinazowakabili ikiwemo wafanyabiashara kutosajili biashara zao.<\/p><p>Samabamba na hayo aliongeza kuwa wapo wafanyabiashara ambao wamesajiliwa kuwa walipakodi lakini wamekuwa hawatii sheria za Kodi hali inayopelekea Serikali kutokusanya mapato yake.<\/p><p>Hivyo Mkurugenzi Saadat aliahidi kuwa ZRA itaendelea na mkakati wake wa kutoa elimu kwa wananchi na wafanyabiashara ili wananchi waelewe umuhimu wa kulipa kodi kwa Maedneleo ya Zanzibar na hatimae ZRA iweze kufikia lengo la Makusanyo lililowekwa na Serikali.<\/p><p>Jumla ya Mamlaka Sita (6) za Kodi kutoka baadhi ya Nchi Wanachama wa Jumuiya ya Afrika Mashariki ikiwemo Kenya, Burundi, Tanzania (TRA &amp; ZRA), Rwanda na Sudani ya Kusini zinashiriki Mkutano huo wa Siku tano (5) ambao umeanza leo na unatarajiwa kumalizika Ijumaa 31\/01\/2025.<\/p>","protected":false},"excerpt":{"rendered":"<p>Na Muandishi Wetu. MAMLAKA za Kodi za nchi za Afrika Mashariki, zimesema zitaendelea kushirikiana pamoja katika kutatua changamoto za kodi zinazofanana na kubadilishana uzoefu ambao utasaidia kuimarisha mapato ya nchi zao. Kaimu Kamishna Mkuu wa Mamlaka ya Mapato Zanzibar (ZRA) Ndg. Saidi Ali Mohamed, alieleza hayo leo wakati akifungua mkutano wa 98 wa Kamati ya [&hellip;]<\/p>","protected":false},"author":1,"featured_media":7467,"comment_status":"open","ping_status":"open","sticky":false,"template":"","format":"standard","meta":{"_monsterinsights_skip_tracking":false,"_monsterinsights_sitenote_active":false,"_monsterinsights_sitenote_note":"","_monsterinsights_sitenote_category":0,"footnotes":""},"categories":[103],"tags":[],"class_list":["post-7589","post","type-post","status-publish","format-standard","has-post-thumbnail","hentry","category-news"],"aioseo_notices":[],"_links":{"self":[{"href":"https:\/\/website.zanrevenue.org\/sw\/wp-json\/wp\/v2\/posts\/7589","targetHints":{"allow":["GET"]}}],"collection":[{"href":"https:\/\/website.zanrevenue.org\/sw\/wp-json\/wp\/v2\/posts"}],"about":[{"href":"https:\/\/website.zanrevenue.org\/sw\/wp-json\/wp\/v2\/types\/post"}],"author":[{"embeddable":true,"href":"https:\/\/website.zanrevenue.org\/sw\/wp-json\/wp\/v2\/users\/1"}],"replies":[{"embeddable":true,"href":"https:\/\/website.zanrevenue.org\/sw\/wp-json\/wp\/v2\/comments?post=7589"}],"version-history":[{"count":1,"href":"https:\/\/website.zanrevenue.org\/sw\/wp-json\/wp\/v2\/posts\/7589\/revisions"}],"predecessor-version":[{"id":7591,"href":"https:\/\/website.zanrevenue.org\/sw\/wp-json\/wp\/v2\/posts\/7589\/revisions\/7591"}],"wp:featuredmedia":[{"embeddable":true,"href":"https:\/\/website.zanrevenue.org\/sw\/wp-json\/wp\/v2\/media\/7467"}],"wp:attachment":[{"href":"https:\/\/website.zanrevenue.org\/sw\/wp-json\/wp\/v2\/media?parent=7589"}],"wp:term":[{"taxonomy":"category","embeddable":true,"href":"https:\/\/website.zanrevenue.org\/sw\/wp-json\/wp\/v2\/categories?post=7589"},{"taxonomy":"post_tag","embeddable":true,"href":"https:\/\/website.zanrevenue.org\/sw\/wp-json\/wp\/v2\/tags?post=7589"}],"curies":[{"name":"wp","href":"https:\/\/api.w.org\/{rel}","templated":true}]}}