
ZRA Yarejesha Fadhila kwa Jamii
DC Hamida Apigilia Msumari Risiti za Kielektroniki Na. Muandishi Wetu. Mkuu wa Wilaya ya Magharibi “B” Mhe. Hamida Mussa Khamis amesema maisha na ustawi wa wananchi yanategemea sana kodi ili Serikali iendelee kutekeleza miradi mbalimbali ya Maendeleo. Ameyasema hayo leo alipokuwa Mgeni Rasmi wakati wa hafla ya kutoa msaada wa Vyakula kwa Wananchi wenye mahitaji maalumu kutoka Shehia mbalimbali za Wilaya ya Magharibi “B”, Msaada huo umetolewa na Mamlaka ya Mapato Zanzibar (ZRA). Mhe. Hamida amesema Serikali imekuwa ikihimiza Wafanyabiashara kulipa kodi kwa hiyari sambamba na kuwahamasisha Wananchi kudai Risiti za Kielektroniki ili kodi halisi ya Serikali





