Muda wa kazi: Mon - Fri 8.00 am - 5.00 pm

MAMLAKA YA MAPATO ZANZIBAR

"Tulipe Kodi kwa Maendeleo ya Zanzibar"

FAQ - Frequecy Asked Question

Maswali na Majibu

ZRA ni taasisi ya kodi inyosimamia kodi zisizokuwa za muungano ambazo hukusanywa kupitia vianzio vya ndani vya biashara ikiwa Pamoja na kodi za ongezeko la Thamani (VAT), kodi ya Ushuru wa stempu ,Ushuru wa hoteli na nyenginezo, ambapo Mamlaka ya mapato Tanzania (TRA) hukusanya kodi zote za mapato (Income Tax)Pamoja na Ushuru wa Forodha.

Aidha Mapato yote yanayokusanywa na mamlaka ya mapato Tanzania (TRA) Afisi ya Zanzibar Pamoja nayanyokusanywa na mamlaka ya mapato Zanzibar huingizwa katika Mfuko mkuu wa Hazina ya serikali ya mapinduzi ya Zanzibar kwa ajili ya matumizi ya miradi ya maendeleo ya Zanzibar na wananchi wake .

ZRA,TRA,Halimashauri ,Manispaa na Baraza la Mji zote ni taasisi hizi zinamnasaba katika majukumu yao kwa kuwa kazi kubwa ni ukusanyaji wa mapato ya serikali .Tofauti kubwa ni kuwa ZRA na TRA zinasimamia mapato ya serikali kuu na tasisi nyengine zilizobaki zinasimamiwa na Halimashauri ,Manspaa au Baraza la Mji.

ZRA hukusanya kodi za ndani kupitia vianzio vya ndani vya biashara zote zinazofanyika Zanzibar ambapo TRA hukusasha kodi zinazotokana na kipato ,Halmashauri/Manspaa/Baraza la Mji hukusanya ada au tozo mbali mbali kupitia vianzio mbali mbali vya mapato katika maeneo yao na kuwapatia Wananchi huduma kulingana na mahitaji ya eneo husika .

Ada au tozo hizo hukusanywa kupitia vianzio kama maegesho ,minada, ada za usafi ,vibali vya ujenzi ,ada za leseni nakadhalika.

Kutoka na muundo wan chi yetu ambayo ni jamuhuri ya Tanzania ,moja ya mambo ya msingi ya Muungano ni kodi ya Mapato na ushuru wa Forodha, ambayo imeeleza katika katiba ya Jamuhuri ya muungano wa Tanzania .Hivyo , Zanzibar kuna Afisi za Mamlaka ya mapato Tanzania (TRA) ambazo hukusanya kodi zenye sura ya Muungano kwa upande wa Zanzibar au kodi nyengine zilizoelekezwa kwa mujibu wa sheria ,kodi ambazo huingia katika hazina kuu ya Serikali ya mapinduzi ya Zanzibar.

Aidha,Tanzania Bara hakuna Afisi za ZRA kwasababu ZRA kwa mujibu wa sheria inawajibika kukusanya mapato ya ndani ya visiwa vya Zanzibar pekee.

JIBU

Leseni ya Tanzania bara inweza kutumia Zanzibar iwapo itasibitishwa na Mamlaka ya Usafiri na Leseni ya Zanzibar kwa kupatiwa kibali maalum cha matumizi ya Leseni hiyo ambayo itatumika kwa muda wa siku (90).

Tanbihi:kibali kitakapomaliza muda wake mmiliki wa Leseni atapaswa kusajili Leseni ya Zanzibar kwa kufuata taratibu za upatikanaji wa leseni hiyo.

JIBU

  • Kuwa na eneo maalumu linalotambulika la biashara .

  • Nakala ya kitambulisho cha Mzanzibari Mkazi/kitambulisho cha Taifa /Hati ya kusafiria.

  • Mauzo ya biashara yaane million 5 kwa mwaka.

  • Kuwa na leseni ya biashara kutoka Manispaa husika.

  • Picha mbili (2) aina ya passpoti size za mmiliki wa biashara.

  • Kopi ya cheti ya TIN kutoka TRA.

  • Kopi ya leseni ya biashara.

  • Kopi ya mkataba wa kukodi eneo la biashara /Lease Agreement.

  • Kujaza fomu ya kuomba usajili wa mlipa kodi.

  • Kopi ya usajili wa jina la biashara.

JIBU

Ankara ya kodi ni waraka wa kisheria unaotolewa kabla ya malipo ya bidhaa au huduma .Wakati Risiti ni waraka maalum wa kisheria unatolewa baada ya mauzo kukamilika na fedha kulipwa.

Tofauti kati ya Ankara ya kodi na Risiti ,Ankara ya kodi ni waraka wa kisheri utolewao na mlipakodi ambae amesajiliwa na kodi ya ongezeko la Thamani (VAT) kila anapofanya mauzo bidhaa/huduma .Ambapo Risiti ni waraka kisheria utolewa na mlipakodi aliyesajiliwa na Ushuru wa Stempu (stamp duty) au kodi nyengine isiyokuwa ya VAT.

JIBU

Kwa kawaida Leseni za udereva huwa na uhai wa kuanzia miaka miwili (2),mitatu(3) au mitano(5).Aidha Leseni hizo zinapomaliza muda wake wa matumizi mmiliki anaweza kufika Afisi za ZRA si Zaidi ya miaka mitatu tangu leseni hiyo ilipo maliza muda wake .Iwapo itafika miaka mitatu bila ya leseni hiyo kuongezwa muda wa matumizi ,leseni hiyo itafutwa na mmiliki atalazimika kuanza upya taratibu za kupata leseni ya udereva iwapo atahitaji kuwa na leseni ya udereva.

JIBU

Kuhusu umiliki wa chombo cha moto ,ni lazima kwa kila chombo cha moto kuwa na usajili jina la mmiliki halali kwa muda husika .Ikiwa kumefanyika mabadiliko ya umiliki kutoka kwa mmiliki mmoja Kwenda mmiliki mwengine, wahusika wanapaswa kufika ZRA na kushukuwa fomu ya umiliki wa chombo .

Pamoja na fomu iliyojazwa na wahusika hao , wataambatanisha nakala za vitambulisho vya utaifa Pamoja na Kadi ya chombo husika na kuviwasilisha vitu hivyo katika Afisi ya Msajili wa Wakala wa Usajili waMali na Biashara (BPRA) kwaajili ya kubadilisha umiliki .

Baada ya kukamilisha taratibu katika Afisi ya (BPRA),wahusika watapaswa kuwasilisha ZRA nyaraka watakazopatiwa na Afisi ya BPRA kwa ajili ya kuwapatia kadi ya umiliki wa chombo .Gharama zinazopaswa kulipwa kwa kubadilisha umiliki wa Gari ni 50,000TZS,na 25,000TZS kwa ajili ya kubadilisha umiliki wa chombo cha maringi mawili.

"Tulipe Kodi kwa Maendeleo ya Zanzibar"

Ramani

Contact Details

P. O, BOX 2072, Mazizini- Zanzibar
Opening Hours:
Mon – Fri: 8:00 am – 5:00 pm

ZRA News & Updates

The latest ZRA news, articles, and resources, sent straight to your inbox every month.

Zanzibar Revenue Authority - © 2025. All Rights Reserved

“Tulipe Kodi kwa Maendeleo ya Zanzibar”

0