Muda wa kazi: Mon - Fri 8.00 am - 5.00 pm

MAMLAKA YA MAPATO ZANZIBAR

"Tulipe Kodi kwa Maendeleo ya Zanzibar"

ZRA Yarejesha Fadhila kwa Jamii

DC Hamida Apigilia Msumari Risiti za Kielektroniki

Na. Muandishi Wetu.

Mkuu wa Wilaya ya Magharibi “B” Mhe. Hamida Mussa Khamis amesema maisha na ustawi wa wananchi yanategemea sana kodi ili Serikali iendelee kutekeleza miradi mbalimbali ya Maendeleo.

Ameyasema hayo leo alipokuwa Mgeni Rasmi wakati wa hafla ya kutoa msaada wa Vyakula kwa Wananchi wenye mahitaji maalumu kutoka Shehia mbalimbali za Wilaya ya Magharibi “B”, Msaada huo umetolewa na Mamlaka ya Mapato Zanzibar (ZRA).

Mhe. Hamida amesema Serikali imekuwa ikihimiza Wafanyabiashara kulipa kodi kwa hiyari sambamba na kuwahamasisha Wananchi kudai Risiti za Kielektroniki ili kodi halisi ya Serikali iweze kukusanywa na hatimaye kuwarudia Wananchi kwa Miradi mbalimbali ya Maendeleo ikiwemo ujenzi wa Skuli za kisasa, Hospitali za Wilaya, Miundombinu ya Barabara, Miradi ya Maji na miradi mengineyo.

Akizungumzia kuhusu Sadaka iliyotolewa na ZRA Mkuu wa Wilaya Hamida amesema Sadaka hiyo imezingatia makundi mbalimbali ya wenye uhitaji katika jamii ndani ya Mwezi Mtukufu wa Ramadhan kama vile wazee wasiojiweza, watu wenye ulemavu, watoto yatima, wajane bila ya kuwasahau watu wanaoishi katika mazingira magumu.

Sambamba na hayo alibainisha kuwa ni vyema Wananchi wakatilia mkazo suala la kuhamasishana kulipa kodi kwani Kodi ndio chachu ya kuongeza Mapato ya Serikali na hatimae huipa uwezo Serikali wa kufikisha huduma kwa jamii huku akitolea mfano msaada uliotolewa na ZRA kwa Wananchi hao.

Mbali na Hayo Bi. Hamida ameipongeza Mamlaka ya Mapato Zanzibar kwa kuendelea kukusanya kodi kwa ufanisi sambamba na kurejesha kwa jamii sehemu ya kile wanachokikusanya kupitia utoaji wa misaada mbalimbali kwa jamii.

Kwa upande wake Meneja wa Mkoa wa Magharibi Kikodi kutoka ZRA Ndg. Maryam Abdalla Balozi akimuwakilisha Kamishna Mkuu wa ZRA Ndg. Said Kiondo Athumani, amesema ni kawaida kwa ZRA kila inapofika mwezi mtukufu wa Ramadhan kutoa sadaka kwa wenye uhitaji ili nao waweze kupata futari kama watu wengine wenye uwezo.

Aidha, amewaomba wafanyabiashara kulipa kodi kwa hiyari huku akiwasisitiza Wananchi kudai Risiti za Kielektroniki kila wanapofanya manunuzi ili Serikali ya Awamu ya nane inayoongozwa na Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mhe. Dkt. Hussein Ali Mwinyi iweze kuzitumia Kodi zinazokusanywa kwa ajili ya kuwaletea Maendeleo wazanzibari.

Akizungumza kwa niaba ya Wananchi wa Shehia tano za Wilaya ya Maghahribi “B” zilizopatiwa msaada na ZRA Sheha wa Shehia ya Bweleo Ndg. Mataka Makame Mataka ameipongeza ZRA kwa kutoka sadaka kwa watu wenye uhitaji katika jamii huku akiwaomba wananchi hao kuwa mabalozi wa kuhamasisha ulipaji kodi wa hiyari.

Baadhi ya Wananchi kutoka Shehia tano za Wilaya ya Magharibi “B” ambazo ni Shehia ya Kisauni, Shehia ya Maungani, Shehia ya Nyamanzi, Shehia ya Kisauni na Shehia ya Bweleo wamepatiwa misaada ya Vyakula na ZRA inayojumiusha Mchele, Sukari, Unga wa Nagno na Mafuta ikiwa ni sehemu ya kurejesha fadhila kwa jamii.

Previous Rais Mwinyi Amuapisha Bosi Mpya ZRA

Leave Your Comment

"Tulipe Kodi kwa Maendeleo ya Zanzibar"

Ramani

Contact Details

P. O, BOX 2072, Mazizini- Zanzibar
Opening Hours:
Mon – Fri: 8:00 am – 5:00 pm

ZRA News & Updates

The latest ZRA news, articles, and resources, sent straight to your inbox every month.

Zanzibar Revenue Authority - © 2025. All Rights Reserved

“Tulipe Kodi kwa Maendeleo ya Zanzibar”

0