Muda wa kazi: Mon - Fri 8.00 am - 5.00 pm

MAMLAKA YA MAPATO ZANZIBAR

"Tulipe Kodi kwa Maendeleo ya Zanzibar"

Rais Mwinyi Amuapisha Bosi Mpya ZRA

Rais Mwinyi Amuapisha Bosi Mpya ZRA

  • CG Kiondo Abainisha Atinga Mikakati yake

RAIS wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mhe. Dkt. Hussein Ali Mwinyi amemuapisha Kamishna Mkuu mpya wa Mamlaka ya Mapato Zanzibar (ZRA) Ndg. Said Kiondo Athumani.
Hafla ya uapisho huo imefanyika leo Ikulu Zanzibar na kuhudhuriwa na viongozi mbalimbali akiwemo Makamu wa Pili wa Rais Mhe. Hemed Suleiman Abdulla, Mwanasheria Mkuu wa Serikali Dkt. Mwinyi Talib Haji, Jaji Mkuu wa Zanzibar Mhe. Khamis Abdalla Shaaban, Kadhi Mkuu wa Zanzibar Othman Ngwali, Makamanda wa Vikosi vya SMZ na viongozi wengine wa chama na Serikali.

Akizungumza mara baada ya uapisho huo, Kamishna Said alimpongeza Rais Mwinyi kwa kumuamini kumpa kazi ya kumsaidia katika kukusanya mapato ya serikali kupitia ZRA.

Alisema kazi hiyo inahitaji mipango na mikakati ya kutosha kwani baadhi ya wafanyabiashara wako tayari kukwepa kodi ya Serikali hali inayopelekea ugumu katika ukusanyaji wa kodi hizo.

Sambamba na hayo alibainisha kuwa suala la kulipa kodi ni wajibu kwani kodi inasaidia kuleta maendeleo katika nyanja mbalimbali ikiwemo sekta ya elimu, sekta ya afya na Sekta ya Miundombinu hivyo amesisitiza wafanyabaishara kuendelea kulipa kodi ili waendelee kushuhudia Serikali ikifanya maendeleo kupitia kodi zao.

Aidha ameongeza kuwa ZRA itahakikisha inakaa na walipa kodi ili kuwahimiza, kuwafundisha, kuwashawishi na kutumia utaalamu walionao ili wafanyabiashara waweze kulipa kodi kwa hiari.

Naye Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais Fedha na Mipango Mhe. Dkt. Saada Mkuya Salum, alisema ZRA imekuwa ikifanya vizuri katika ukusanyaji wa mapato na mafanikio hayo yanatokana na mageuzi makubwa yaliyofanyika ikiwemo matumizi ya mifumo ya Kielektroniki katika ukusanyaji wa Mapato.

Alisema awali yalikuwepo mambo ambayo yalikuwa yakiifanya taasisi hiyo kutofanya vizuri zaidi ikiwemo baadhi ya watumishi kutokuwa waaminifu na waadilifu katika utendaji wa kazi zao.

 Waziri Saada alisema mambo hayo yote yameondoka na kwa sasa wastani wa makusayo ya ZRA yanapindukia zaidi ya asilimia 100 ambayo ni mafanikio makubwa kwa taasisi hiyo ya ukusanyaji Mapato Zanzibar.

Ikumbukwe kuwa Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mhe. Dkt. Hussein Ali Mwinyi alimteuwa ndugu Said Kiondo Athumani Febuari 8 mwaka huu kuwa Kamishna Mkuu wa ZRA baada ya aliyekuwa Kamishna Mkuu wa Mamlaka hiyo Ndg. Yussuph Juma Mwenda kuteuliwa na Rais wa Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania kuwa Kamishna Mkuu wa Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA) Julai 2, 2024.

Previous ZRA Yakabidhiwa Kombe la Zanzibar Heroes

Leave Your Comment

"Tulipe Kodi kwa Maendeleo ya Zanzibar"

Ramani

Contact Details

P. O, BOX 2072, Mazizini- Zanzibar
Opening Hours:
Mon – Fri: 8:00 am – 5:00 pm

ZRA News & Updates

The latest ZRA news, articles, and resources, sent straight to your inbox every month.

Zanzibar Revenue Authority - © 2025. All Rights Reserved

“Tulipe Kodi kwa Maendeleo ya Zanzibar”

0